Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sambamba na Mawkibu za kuwahudumia Mahujaji / Mazuwwari wa Arubaini, pia kuna idadi ndogo ya Mawkibu za kitamaduni zilizo kwenye njia ya matembezi ya Arubaini na ndani ya mji wa Karbala. Wajibu mkubwa wa Mawkibu hizi za kitamaduni katika hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu na wakati wa kuzingirwa kwa watu wa Gaza ni kufafanua ukweli na kutetea harakati za Muqawama (upinzani wa haki).
Abu Ali, mwenye Mawkibu ambaye ni Iraq, akieleza kuhusu mipango ya elimu na uhamasishaji kwenye Mawkibu yake sambamba na huduma kwa mahujaji / Mazuwwari wa Arubaini, alisema katika mahojiano na ABNA:
"Nachukua fursa hii kuwapa pole kwa kuwadia kwa siku za Arubaini ya Imam Hussein (a.s). Shughuli zetu za Arubaini zinahusiana na banda lililo Karbala ambalo linatoa huduma za kielimu na uhamasishaji kwa mahujaji / Mazuwwari wa Arubaini wakiwemo Wairaq, Wairan, Walebanon, na watu wengine kutoka mataifa mbalimbali."
Aliendelea kusema: "Wahudumiwa katika banda letu wanatoka makundi yote ya kijamii na mataifa tofauti. Tunajitahidi kubainisha masuala muhimu. Tunafanya Jihadi ya Kuelimisha kwa kufikisha sauti ya dhulma wanayopata mataifa ya Iran, Iraq, Palestina, Lebanon, na Yemen. Kwa hakika, tupo pamoja na upinzani dhidi ya wavamizi Wamarekani na Wazayuni."
Mwenye Moakibu huyu aliongeza: "Katika vita vya siku 12 tulikuwa pamoja na Jamhuri ya Kiislamu kupinga mashambulizi ya kinyama ya Israel, na leo, kesho, na daima tutaendelea kusimama na muqawama, Insha-Allah."
Akizungumzia vita hivyo, alisema: "Vita vya Israel dhidi ya Iran vilikuwa vya kinyama, lakini Iran ilijibu kwa haki kupitia makombora yake dhidi ya uvamizi huo, na bila shaka Iran itashinda kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu inasimama kulinda Uislamu Safi wa Muhammad (s.a.w.w.) chini ya uongozi wa Ayatullah Khamenei (h), mrithi wa Imam Ruhullah Khomeini (r.a.)."
Abu Ali aliongeza: "Alhamdulillah tunaona umoja mkubwa kati ya mitazamo ya Wairani na Wairaqi katika kupambana na adui, kupinga ugaidi, kupinga dhulma na siasa za kuwanyima chakula watu wa Palestina, hasa wa Gaza."
Amesisitiza: "Tumeungana na Jamhuri ya Kiislamu na Insha-Allah tutaendelea kuwa wamoja siku zijazo. Iraq na Iran ni taifa moja lililo imara."
Mwanaharakati huyu wa kitamaduni alisema: "Shughuli zetu za vyombo vya habari zinaendelea mwaka mzima, kuanzia kuchapisha mabango na machapisho kwenye Telegram na Facebook, hadi kushirikiana na wapiganaji wa jihadi ya vyombo vya habari. Tuna uhusiano mzuri na vyombo vya habari vya Hashd al-Shaabi kama vile Nujabaa. Tunabainisha umuhimu wa uwepo wa Hashd al-Shaabi, ambao ni kama ngao imara na mlinzi wa mambo matukufu. Daima tupo pamoja nao na tunapinga kila mtu au kikundi kinachojaribu kuchafua taswira ya Hashd."
Mwisho, akiwa anakumbuka mashahidi viongozi wa muqawama, hasa Shahidi Haj Ramadan aliyekuwa akihusika na masuala ya Palestina, alisema:
"Jamhuri ya Kiislamu Iran daima ipo kwenye mstari wa haki, na sisi pia tutabaki pamoja nayo katika mstari huo na katika njia ya mashahidi, hadi kufanikisha lengo la mwisho ambalo ni kuangamizwa kwa utawala wa Kizayuni, Insha-Allah."
Your Comment